Ecclesiastes 7:3-6

3 aHuzuni ni afadhali kuliko kicheko,
kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo.
4 bMoyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba,
lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa.
5 cAfadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima,
kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
6 dKama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria,
ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.
Hili nalo pia ni ubatili.
Copyright information for SwhNEN